Duniani kuna mambo, tena ya ajabu kweli kweli. Na tena mengi yapo
huko kwenye zile nchi wanazoziita za dunia ya kwanza – kuna vioja vya
kukuacha mdomo wazi.
Vitalii alijipenyeza kwenye umati wengi wa watu kutaka kubusu makalio maarufu ya Kim Kardashian
Jumatano hii, njemba moja, tena maarufu, liitwalo Vitalii Sediuk
lilifanya jambo la hatari,. Mchana kweupe tena katikati ya ulinzi
mkali.. Kipi hicho? Lilitaka kubusu makalio ya Mrs Kanye West, Kim
Kardashian.
Walinzi wa Kim Kardashian wakimzuia Vitalii kutotimiza azma yake
Mtu huyo ambaye amewahi kuwafanyia vimbwanga mastaa wengine, wakiwemo
Brad Pitt na Leonardo DiCaprio, aliushika mguu wa Kim akitaka kubusu
makalio yake lakini walinzi walimuwahi na kumbwaga chini.
Sasa unaelewa kwanini Kim Kardashian anahitaji walinzi wengi
Vitalii ametumia Instagram kueleza kwanini alifanya kioja hicho.
“I was protesting Kim for using fake butt implants. I encourage her
and the rest of Kardashian clan to popularise natural beauty among
teenage girls who follow and defend them blindly,” aliandika!
Cheki video yatukio hilo hapa!
Inasemekana kuwa Kim amefungua mashtaka dhidi yake.
Tukio hilo limekuja wiki moja tu baada ya jamaa huyo huyo kumvamia
mrembo Gigi Hadid kwa kumbeba juu juu huko Milan lakini akaambua bonge
la kipepsi toka kwa mrembo huyo.
Pamoja na kufanya kitendo hicho cha hatari, Vitalii aliendelea kudunda mtaani
Pamoja na kufanya yote hayo Vitalii hajachukuliwa hatua na yupo uraiani akidunda kama kawa!
0 comments:
Post a Comment