>>>’hali imebadilika kwa sababu tuna serikali mpya na ina namna yake ya kufanya shughuli zake, kwa hiyo ni dhahiri kwamba namna ambavyo tulikuwa tunafanya siasa lazima ziwe tofauti na sasa hivi kwa sababu ajenda zimebadilika mfano ni ajenda ya kupambana na ufisadi ilikuwa ndio ajenda kuu ya vyama vya upinzani katika serikali ya awamu ya nne sasa hivi serikali yenyewe ndio inayopambana na ufisadi’
>>>’siasa za sasa hivi zinatakiwa ziwe za utekelezaji zaidi, kama wewe ni mbunge au ni diwani utaonekana ni mwanasiasa mahiri kulingana na namna gani umejibu changamoto za wananchi ambao unawaongoza kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita kwamba ni kwa namna gani unaibua uozo katika utendaji wa serikali kwa hiyo lazima kuwe na mabadiliko kidogo ya namna gani tunafanya siasa zetu’:-Zitto
Tazama video akifafanua zaidi
0 comments:
Post a Comment