VIDEO: Mtoto aliyelazimishwa kuolewa asimulia alivyotoroka ili asiolewe Shinyanga!

Takwimu za ndoa za utotoni duniani zinaonesha Tanzania kuwa moja ya nchi zenye viwango vikubwa vya ndoa katika umri mdogo. Kwa wastani watoto wakike wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Zipo pia takwimu kutoka mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF zinaonyesha kuwa, kwa siku, watoto 16 wanapachikwa mimba za utotoni hapa Tanzania.

Leo September 29 2016 wadau mbalimbali wamekutana kwenye majadiliano yaliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili kazi ya vyombo vya habari katika kupambana na ndoa za utotoni Tanzania, moja ya waliozungumza ni mtoto Fortunate Ezekiel toka Shinyanga amesimulia namna alivyotoroka ili kukwepa kuozwa……….
>>>’siku moja kabla ya harusi nilikuwa natoka kisimani, watu walikuwa wamealikwa kwenye harusi na kulikuwea na ngoma nikakutana na msamaria mwema akanihifadhi nikalala na kesho yake akanipeleka kwenye shirika la Agape wakanihifadhi mpaka sasa hivi ninasoma nipo kidato cha kwanza’:-Fortunate Ezekiel
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment