Video: DIAMOND na Kevin Hart Wakila Bata Pamoja Wikiendi Hii Huko Jijini Las Vegas, USA

Diamond Platnumz ameanza kuonesha kuwa hakubahatisha kwa kauli yake ya aliyowahi kuitoa ya kuhakikisha muziki wake unafika Ulaya na Marekani.
Siku mbili zilizopita staa huyo wa Kidogo alionekana akiwa na mchekeshaji na muigizaji wa filamu maarufu duniani, Kevin Hart mjini Los Angeles baada ya kumaliza kushoot video ya wimbo wake wa Marry You aliomshirikisha Ne-yo.

Wikiendi hii hitmaker huyo wa Kidogo amepost kipande cha video Instagram akiwa na muigizaji huyo wa Central Intelligence kwa mara ya pili wakiwa wanakula bata kwenye mji wa Las Vegas. 
“Oosh! Oosh! Someone gotta call 911…My snapchat is in trouble ….. Cc @kevinhart4real #HartbeatWeekend #Lasvegas,” ameandika Diamond kwenye mtandao huo.

Kwenye video hii Kevin anasikika akisema, “Haiya Hartbeat weekend, turn it up, I took over his [Diamond] snapchat, you see him” na Diamond kudakia , “what you see in Vegas, remain here,” na Kevin kumalizia, “I love him my guy.”
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment