Jana September 29, 2016 Millardayo.com ilikuletea
Hekaheka ya kijana mmoja kutoka Mabibo Hostel jijini Dar es salaam
aliyetobolewa Macho na mtu aliyefahamika kwa jina la Scorpion ambaye kwa
mujibu wa maelezo ya kijana huyo ilidaiwa kuwa anaogopwa sana kutokana
na historia ya matukio aliyokuwa akiyafanya mara kwa mara.
Leo
September 30, 2016 Heka Heka ya Leo Tena kupitia Clouds FM imefuatilia
mkasa huo kiundani zaidi baada ya Geah Habib kufika Buguruni na
kuzungumza na wananchi wa eneo hilo na wengine kukiri kushuhudia tukio
alilofanyiwa kijana huyo lakini walishindwa kutoa msaada kwasababu tu
Scorpion alikuwa na uwezo wa kumdhuru mtu na hatua zisichukuliwe juu
yake.
>>>’Watu
wote wanamuogopa hawakuthubutu kusogea wala kumtetea inasemekana hili
ni tukio lake la tatu…… ila sisi tuna hofu hatuna amani yule akikutamani
umekishwa kwa sababu yeye anavyokufuata watu wote watabaki kuangalia tu
huna mtetezi mpaka jama atakapo jiridhisha:–Mkazi Buguruni
>>>Ni kweli hilo
tukio limetokea na polisi tayari walishachukua hatua kwa maana ya huyo
mtuhumiwa Scorpion jina lake halisi anaitwa Salum Mpepe alikamatwa siku
ya tarehe 12 mwezi wa 9 akawa pale kituo cha polisi Buguruni wakati
upelelezi ukiendelea tarehe 23 mwezi wa 9 alifikishwa mahakami na
kusomewa jinai namba 276 unyang’anyi kwa kutumia silaha, yupo magereza
kesi yake itatajwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016:- Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Salum Hamdani.
KUSIKILIZA FULL STORI UNAWEZA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment